Wednesday, October 17, 2012

Utunzaji midomo kiasili

Utunzaji midomo kiasili
 


MATATIZO mbalimbali yanayoipata midomo (lips) kama vile kukauka, kukatika na hatimaye kuchubuka ni matokeo ya uangalizi/utunzaji duni.
Uangalizi huo duni umekuwa ukisababishwa na  uelewa mdogo wa namna ya utunzaji wa ngozi ya midomo.
Kwa mujibu wa wataalam wa mambo ya urembo, zipo njia nyingi za utunzaji wa midomo “lips”, ambapo katika makala haya nitakuletea namna ya kutunza midomo yako kwa njia ya asili.
Njia hizi za asili huwa hazina madhara kwa mtumiaji na hiyo ndio sababu kubwa ya kukubalika na watu wengi tofauti na zile za kutumia kemikali.
Zifuatazo ni baadhi ya njia hizo ambapo unashauriwa kutumia yeyote utakayopendelea au iliyo rahisi kwako.

Paka  Vaseline au samli katika midomo yako kila unapotaka kulala; hii itasaidia kuzifanya lips zako ziwe na unyevunyevu.
Hakikisha unakunywa angalau gilasi nane za maji ili kuboresha ngozi yako.
Hakikisha unatumia losheni maalum za kupaka katika midomo yako hasa wakati wa baridi.
Tumia majani ya hiliki kwa kusugua katika lips zako; hii itakusaidia kuzifanya ziwe laini zaidi.
Kula matunda na mboga za majani ya kutosha; hii pia itasaidia kuboresha si tu ngozi ya midomo bali ya mwili kwa ujumla.
Sugua ngozi ya lips zako kwa kutumia mswaki na maji ya uvuvugu angalau mara moja kwa wiki; hii itasaidia kuondoa seli zilizokufa katika ngozi ya midomo yako.
Midomo myeusi mara nyingi husababishwa na unywaji wa kupindukia wa chai, kahawa na uvutaji wa sigara hivyo unashauriwa kuepukana na matumizi ya vitu hivi ili kuwa na lips nzuri.
Paka mchanganyiko wa juice ya limao na ‘glycerin’ katika ngozi ya midomo yako kila usiku, acha kwa usiku mzima hadi asubuhi ndipo uoshe, hii itakusaidia kung’arisha midomo yako.
Lainisha ngozi ya midomo yako kwa kupaka tui bubu la nazi katika midomo yako .
Kula matango na karoti kwa wingi, hii itakusaida kulainisha lips zako na kuzifanya ziwe za kuvutia muda wote.
Ni hayo tu kwa leo.

                             Mungu awalinde nyote,Nawapenda sana....!

Jinsi ya kuutunza na kuongezea mvuto uso wako


Uso ni sehemu ya kuonyesha uhalisia kwa mwanamke na unapotaka kujua ni jinsi gani mwanadada au mwanamke anapenda urembo basi utamwangalia usoni.


Kwa mtazamo huo utaona yule mpenda urembo akiwa amepaka baadhi ya vipodozi usoni kwa mfano:- Poda, Lip-Stick, Wanja n.k na utagundua kwamba niliyekutana naye ni mmoja kati ya wanawake wanaopenda urembo.


Leo imekuletea mada ya jinsi unavyoweza kusafisha uso wako na ili uelewe hilo fuata haya yafuatayo:-


a)Penda kuosha uso wako kwa maji safi na salama na ili kujiepusha na mlipuko wa maradhi yatokanayo na maji.


b)Kama uso wako wa mafuta basi tumia maji yenye uvugu vugu, ili kupunguza mafuta usoni mwako na ili kuuwezesha uso kuwa mkavu na kama unasura isiyo kavu, basi nakushauri utumie maji yoyote unayopenda kama ni vugu vugu au ya kawaida.


c)Tumia sabubi yoyote nzuri uitumiayo kunawia uso wako siku zote, ili kuiboresha ngozi ya suo wako.


d)Ila penda kutumia sabuni zisizo kali pindi usafishapo uso wako na itakuepusha na baadhi ya matatizo ambayo wanawake wengi huyapata kwa utumiaji wa sabuni kali.


e)Tumia kitambaa safi na salama au taulo laini lililosafi na salama ili usipate matatizo ya michubuko usoni mwako, kitu kitakachopelekea kutokuwa na ngozi nzuri usoni.


f)Usipende kutumia kilevi cha aina yoyote na kama ni mtumiaji usitumie kupita kiasi, kwani itapunguza uzuri wa sura yako kwani ulevi siku zote ni mbaya hupunguza baadhi ya vitamins mwilini mwa mwanadamu.


g)Pia usipende kutumia sigara si nzuri kwa uboreshaji wa sura yako na afya yako kwa ujumla.


h)Jitahidi usiwe mtu wa kutoka toka sana usiku ili upate muda mrefu wa kupumzika na uzidi kuboresha na kuirutubisha ngozi ya uso wako na kuifanya ipendeze daima.


i)Pia unashauriwa kunywa maji, kula mboga za majani na matunda kwa wingi, na kwa kufanya hivyo utazidi kuonekana ni mwanamke mwenye sura safi, nyororo na iliyo na afya njema na yenye kuvutia daima machoni mwa jamii inayokuzunguka.
              Ni hayo tu kutoka kwangu....

                                                        Mungu awe nanyi jamani i love y'all.