Utunzaji midomo kiasili |
MATATIZO
mbalimbali yanayoipata midomo (lips) kama vile kukauka, kukatika na
hatimaye kuchubuka ni matokeo ya uangalizi/utunzaji duni.
Uangalizi huo duni umekuwa ukisababishwa na uelewa mdogo wa namna ya utunzaji wa ngozi ya midomo.
Kwa
mujibu wa wataalam wa mambo ya urembo, zipo njia nyingi za utunzaji wa
midomo “lips”, ambapo katika makala haya nitakuletea namna ya kutunza
midomo yako kwa njia ya asili.
Njia hizi za asili huwa hazina
madhara kwa mtumiaji na hiyo ndio sababu kubwa ya kukubalika na watu
wengi tofauti na zile za kutumia kemikali.
Zifuatazo ni baadhi ya njia hizo ambapo unashauriwa kutumia yeyote utakayopendelea au iliyo rahisi kwako.
• Paka Vaseline au samli katika midomo yako kila unapotaka kulala; hii itasaidia kuzifanya lips zako ziwe na unyevunyevu.
• Hakikisha unakunywa angalau gilasi nane za maji ili kuboresha ngozi yako.
• Hakikisha unatumia losheni maalum za kupaka katika midomo yako hasa wakati wa baridi.
• Tumia majani ya hiliki kwa kusugua katika lips zako; hii itakusaidia kuzifanya ziwe laini zaidi.
• Kula matunda na mboga za majani ya kutosha; hii pia itasaidia kuboresha si tu ngozi ya midomo bali ya mwili kwa ujumla.
• Sugua
ngozi ya lips zako kwa kutumia mswaki na maji ya uvuvugu angalau mara
moja kwa wiki; hii itasaidia kuondoa seli zilizokufa katika ngozi ya
midomo yako.
• Midomo
myeusi mara nyingi husababishwa na unywaji wa kupindukia wa chai,
kahawa na uvutaji wa sigara hivyo unashauriwa kuepukana na matumizi ya
vitu hivi ili kuwa na lips nzuri.
• Paka
mchanganyiko wa juice ya limao na ‘glycerin’ katika ngozi ya midomo
yako kila usiku, acha kwa usiku mzima hadi asubuhi ndipo uoshe, hii
itakusaidia kung’arisha midomo yako.
• Lainisha ngozi ya midomo yako kwa kupaka tui bubu la nazi katika midomo yako .
|